Kikaro High School ni shule ya serikali yenye mchanganyiko wa wasichana na wavulana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita kwa michepuo yote yaani sayansi na sanaa


Shule ya Sekondari Kikaro ipo mkoa wa Pwani wilaya ya Chalinze katika kata ya Miono.Ukitoka Dar es salaam, panda magari yaendayo Saadani au Mionokatika kituo cha daladala cha MBEZI YA KIMARA nauli ni Tsh 7000/=.Ukitokea barabara ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga unatakiwa kushuka kituo cha Mandera Kibaoni, hapo utasubiria gari nyingine kwa nauliTsh 1000/= na utafikishwa hadi shuleni.Ukitokea barabara ya Morogoro (hasa kwa wanaotokea mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Shinyanga n.k) utashukia kituo cha chalinze kisha utapanda gari nyingine zinazoelekea MIONO kwa nauli ya shilingi 4000/= tu.

1,913 Views